“I should say that happiness is being where one is and not wanting to be anywhere else.” — Michael Frayn
Furaha ni matokeo ya mtu kuwa pale alipo na kutokutaka kuwa sehemu nyingine yoyote.
Mtego mkubwa kabisa kwenye maisha na unaozuia wengi wasiwe na furaha ni kutokuwa pale walipo.
Mtu yupo kwenye kazi lakini mawazo yake hayapo kwenye ile kazi anayoifanya, labda anafikiria kupumzika.
Unapofika wakati wa kupumzika, mawazo yake hayakai kwenye mapumziko hayo, bali kwenye vitu vingine, mfano kufikiria kazi.
Hata hofu na msongo wa mawazo ni matokeo ya mtu kutokuwa pale alipo.
Hofu inakuja pale unapoyafikiria sana mambo ambayo hujayafikia. Kama ungeweka fikra zako zote kwenye kile unachofanya, hofu haipati nafasi.
Kadhalika msongo wa mawazo ni kuangalia na kufikiria mambo mengi kwa pamoja.
Unafanya jambo zaidi ya moja huku ukisumbuliwa na mengine, kama ukiweka fikra zako zote kwenye kitu kimoja ulichochagua kufanya na ukaachana na vingine, utapunguza sana msongo wa mawazo.
Kaa pale ulipo, chagua kufanya kitu kimoja kwa wakati na weka fikra zako zote kwenye kile unachofanya. Hilo litakupa furaha na utulivu mkubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kupunguza maamuzi unayofanya, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/20/2181
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.