“People are our proper occupation, our job is to do them good and put up with them.” – Marcus Aurelius
Jukumu lako kuu kwenye maisha ni watu.
Wajibu wako mkubwa ni kuwatendea vyema na kuweza kuendana nao bila ya kujali wakoje.
Kila kazi au biashara unayofanya, inawalenga watu.
Hivyo unapofanya kazi au biashara yako, lengo lako kuu linapaswa kuwafanya watu kuwa bora zaidi ya walivyokuwa, kutoa thamani zaidi.
Haijalishi unalipwa kiasi gani,
Haijalishi wengine wanafanya nini,
Haijalishi kama mwajiri au bosi anakujali au la,
Wajibu wako mkuu ni kufanya mazuri kwa wale wanaoyegemea kile unachofanya.
Na unapofanya siyo kwa ajili ya wale wanaotegemea unachofanya, bali ni kwa ajili yako mwenyewe.
Maana unapofanya vizuri, unajijengea sifa ambayo inakupa fursa nzuri zaidi baadaye.
Kwa kila unachofanya, wajue unaowagusa na kazana kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Hiyo ndiyo njia pekee ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu maoni na ukweli, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/26/2187
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Jukumu letu kwa kila tunachofanya ni kwa ajili ya watu, muhimu ni kuendelea kuwekeza ktk hili.
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike