Simba hata awe na njaa kiasi gani, huwa hawindi panya au wanyama wengine wadogo wadogo. Badala yake anapambana mpaka apate kitoweo sahihi kwake, ambacho ni mnyama mkubwa.

Moja ya kikwazo cha mafanikio kwa wengi ni kushindwa kujiwekea viwango vya juu na kupambana kuvifikia.

Kama unahangaika na kila kitu, hasa vitu vidogo vidogo, huwezi kupata muda wa kuhangaika na yale makubwa yanayokupa mafanikio.

Leo tafakari ni panya gani umekuwa unakimbizana nao (malengo madogo na yasiyokufikisha kwenye mafanikio) kisha achana nayo na hangaika na malengo yaliyo sahihi kwako.

Nguvu unazotumia kuhangaika na yasiyo sahihi, ndiyo nguvu unazojipunja kwenye kuhangaikia yaliyo sahihi.

Jifunze kwa simba kwenye kujiwekea viwango vya juu na kuvisimamia, ndiyo njia ya kufika kwenye mafanikio makubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma

#AfyaUtajiriHekima

#KaziUpendoHuduma.

Kocha.