
Pesa ni zao la thamani. Kiasi cha pesa unachoingiza sasa ni matokeo ya thamani unayozalisha kwa wengine. Kama unataka kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa, toa thamani kubwa zaidi ya unayotoa sasa.
Iwe ni kwenye ajira au biashara, zalisha thamani kubwa zaidi kwa wale wanaotegemea unachofanya. Fanya kwa namna ambayo hakuna mwingine anaweza kufanya.
Kadiri unavyofanya kitu cha kipekee na ambacho kina manufaa kwa wengine, ndivyo wanavyokuwa tayari kukulipa zaidi.
Lengo lolote la kuongeza kipato ulilonalo, linapaswa kuanzia kwenye thamani unayozalisha.
Fanya kinachofanywa na wengi na utalipwa kidogo. Fanya kisichoweza kufanywa na wengi na utalipwa zaidi.
Kila unachofanya jiulize wengine wananufaikaje na angalia nani wengine wanaweza kufanya. Fanya chenye thamani kubwa na kisichoweza kufanywa na wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma.
Kocha.
Asante kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike