Wakati pekee ambao nina udhibiti nao ni wakati uliopo. Siku pekee ninayoweza kuitumia kufanya makubwa ni siku hii ya leo. Jana imeshapita, chochote nilochofanya au kushindwa kufanya siwezi kukibadili. Kesho bado haijafika, chochote ninachohofia kuhusu hiyo kesho siwezi kukiathiri. Lakini leo, iko kwenye mikono yangu, ipo ndani ya udhibiti wangu, naweza kuitumia nitakavyo. Nitaitumia siku ya leo kufanya yake muhimu kwangu, nitajiwekea vipaumbele na kuvifuata hivyo. Najua muda wangu ni wa thamani mno, sitaupoteza kwa chochote kisicho muhimu. Leo ni siku yangu, leo nakwenda kufanya makubwa. #NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma