‎Unapoteza Masaa 1,095 Kila Mwaka…Bila Hata Kujua…!
‎
‎Rafiki Yangu,
‎
‎Hebu fikiria hili.
‎
‎Masaa matatu (3) kila siku.
‎Dakika 180.
‎Yaani muda wa kuangalia status, reels, ku-scroll bila mpango.
‎
‎Ukijumlisha kwa mwaka mzima?
‎Unapata Masaa 1,095.
‎Sawa na siku 45 mfululizo.
‎
‎Mwezi mmoja na nusu wa maisha yako.
‎Umeyatoa bure.
‎Bila hata kushtuka.
‎
‎Tatizo si kwamba huna muda.
‎Tatizo ni huujui unaenda wapi.
‎
‎Unaamka mapema.
‎Una shughuli nyingi.
‎Una majukumu.
‎
‎Lakini mwisho wa siku unasema,
‎Leo sijafanya kitu cha maana.
‎Unajua kwanini?
‎
‎Kwa sababu muda wako unaendeshwa na kila kitu isipokuwa wewe.
‎Simu inakuita.
‎Watu wanakuita.
‎Taarifa zinakuvuta.
‎
‎Na wewe unafuata.
‎Hakuna ratiba.
‎Hakuna mipaka.
‎
‎Hakuna uamuzi wa makusudi.
‎Na kama wewe ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mwanafunzi, au mzazi…
‎
‎Hili linakuuma zaidi.
‎Kwa sababu ndoto zako zinahitaji muda.
‎Lakini muda wako unaibiwa kimya kimya.
‎
‎Fikiria hili kwa sekunde moja.
‎Masaa 1,095 kwa mwaka.
‎Kwa miaka 5?
‎
‎Masaa 5,475.
‎
‎Hiyo ni zaidi ya miezi 7 ya maisha yako.
‎Imetoweka.
‎Bila kujenga biashara.
‎Bila kusoma kitabu.
‎Bila kuongeza kipato.
‎
‎Bila kusogea karibu na ndoto zako.
‎Halafu unajiuliza,
‎Kwanini maisha yangu hayasogei?
‎
‎Unahisi umechoka kila siku.
‎Lakini si kazi inayokuua.
‎Ni muda uliotumika vibaya.
‎
‎Na kitu kibaya zaidi?
‎Hujawahi kukaa chini kuuhesabu.
‎Unaishi kwa mazoea.
‎
‎Unasukumwa na mazingira.
‎Sio wewe unayeongoza muda.
‎Muda ndio unakuongoza.
‎
‎Sikiliza vizuri.
‎Watu wengi wanafikiri suluhisho ni kuamka saa 10 alfajiri.
‎Au kuongeza bidii.
‎
‎Au kusukuma masaa mengi zaidi.
‎
‎Hapana.
‎Hilo silo suluhisho.
‎
‎Kama huna mfumo wa muda,
‎Hata ukiamka saa 9 usiku,
‎Bado utapoteza masaa.
‎
‎Kinachokosekana si juhudi.
‎Ni mpangilio.
‎Ni kujua:
‎Nini kifanyike.
‎Kifanyike lini.
‎Kwa muda gani.
‎
‎Na nini kisifanyike kabisa.
‎
‎Ukikosa hilo,
‎Utaendelea kupoteza Masaa 1,095 kila mwaka.
‎
‎Ndiyo maana kimeandikwa kitabu kizuri cha MUDA UPO.
‎Hiki si kitabu cha nadharia.
‎Ni mwongozo wa vitendo.
‎
‎Kinakuonyesha:
‎• Jinsi ya kugawa siku yako kimkakati.
‎• Jinsi ya kuondoa vitu vinavyokuibia muda.
‎• Jinsi ya kuweka vipaumbele vinavyozalisha matokeo.
‎• Jinsi ya kuishi siku moja yenye maana.
‎Ukisimamia siku moja vizuri,
‎
‎Wiki itanyooka.
‎Mwezi utanyooka.
‎Mwaka utabadilika.
‎
‎Muda hauongezeki.
‎Lakini ukipangiliwa vizuri,
‎Unatosha.
‎
‎Ndiyo maana kinaitwa MUDA UPO.
‎Kwa sababu kweli upo.
‎Tatizo ni hujui kuutumia.
‎
‎Kama wewe ni mtu wa ndoto kubwa…
‎Hii si habari ya kupuuza.
‎Kama unataka kuongeza kipato chako.
‎
‎Basi anza na hiki kitabu, unakipata hapa 👇 karibu.
‎
‎https://wa.link/qb711b
‎Karibu.
‎0756694090.