Kila siku mpya unayoianza, unakuwa na nguvu na muda ambao ni sawa.

Unapoimaliza siku hiyo, unakuwa umetumia muda na nguvu ulizoanza nazo. Iwe umefanya mambo mazuri na ya mafanikio au umefanya mambo ya hovyo haijalishi, muda na nguvu vitakuwa vimetumika.

Muda na nguvu utakazotumia kuzurura mitandaoni, au kubishana au kufuatilia maisha ya wengine ni muda na nguvu ambazo ungeweza kutumia kujifunza zaidi kile unachofanya, kuweka ubora zaidi, kutafuta na kuwahudumia wateja zaidi.

Kabla ya kutumia muda na nguvu zako, jiulize kama unachofanya ni kitu chenye manufaa na kukufikisha kwenye mafanikio. Kama siyo basi usifanye.

Rasilimali hizo mbili ni muhimu na zenye ukomo, zichunge mno, maana usipozijali na kuzitumia kwa manufaa yako, wengine wataziiba na kuzitumia kwa manufaa yao.

Kwa kuwa utazitumia rasilimali hizo kila siku, basi hakikisha unazitumia kwa yaliyo muhimu tu. #NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma