
Tunategemeana sana kwenye maisha, hakuna anayeweza kushinda peke yake. Ushindi wa mwalimu ni wanafunzi wanaofaulu, ushindi wa daktari ni wagonjwa wanaopona na ushindi wa mpishi ni watu wanaoshiba na kufurahia chakula.
Chochote unachofanya, angalia wale unaowalenga wananufaikaje, wajibu wako ni kuhakikisha wanashinda, maana wakishinda hao, ndiyo na wewe unashinda pia.
Kwa kila unachofanya, usiangalie tu wewe unapata nini, bali angalia pia wengine wananufaikaje, ni ushindi gani unawasaidia wengine kupata.
Ni watu gani unaokwenda kuwapa ushindi leo? Hao ndiyo wenye mafanikio yako, wajue na leo nenda kapambane wapate ushindi.
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuwasaidia wengine kushinda, fungus hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/12/2204
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma