Nimekuwa naandika mara nyingi kuhusu fedha na hapa nimekusanya yale muhimu unayopaswa kuyajua kila wakati kuhusu fedha. Siyo mapya, ila ni ya kujisisitizia uyaelewe kwa undani.
Ongeza kipato chako, kila wakati pambana kukiongeza.
Dhibiti matumizi yako, yasikue kuzidi kipato.
Kuwa na akiba ya dharura angalau miezi 6 mpaka 12 ya kuweza kuendesha maisha yako hata kama huingizi kipato.
Fanya uwekezaji endelevu, unaozalisha faida na unaokua kwa thamani.
Kuwa na malengo ya kifedha unayofanyia kazi, kwenye ukuaji wa kipato, udhibiti wa matumizi (bajeti), akiba ya dharura na uwekezaji.
Wapende na wakubali wale wenye fedha zaidi yako, ujifunze kwao jinsi ya wewe kupata fedha zaidi.
Unalipwa kulingana na thamani unayozalisha, kulipwa zaidi zalisha thamani zaidi kwa wengi zaidi.
Thamani isiyo na ushindani unayoweza kuzalisha ni kuwa wewe na kufanya kile ambacho hakuna mwingine anaweza kufanya.
Jua hisia zinazokusukuma kifedha na zitumie kwa namna iliyo bora.
Usishindane na wengine kifedha, iwe ni kwenye kipato au matumizi.
Kuwa na vyanzo vingi vya kipato, usitegemee eneo au sekta moja pekee.
Tawanya uwekezaji wako, usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja.
Kuwa tayari kupoteza kila kitu na kuanza upya, usishikize utu wako kwenye pesa au mali zako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,