Kama mtu amekukasirisha na kisha ukamtukana, tatizo siyo hasira ambayo umekuwa nayo, bali tatizo ni matusi yaliyo ndani yako.

Huwezi kutoa kitu ambacho hakipo ndani yako. Kama hujui kuongea lugha ya kichina, hata ukasirishwe kiasi gani, hutaiongea, kwa sababu haipo ndani yako.

Kwa mambo yote unayofanya au kusema na baadaye kuja kujutia na kuona labda ni hasira, hisia au ulevi vimepelekea usema au kufanya mambo hayo, jua shida siyo vitu hivyo, bali shida ni wewe mwenyewe.

Kinachokuwa kimetokea ni umejikuta kwenye hali ambayo huwezi tena kuigiza au kujizuia, hivyo yaliyojaa ndani yako yanaanza kumwagika.

Chochote unachotoa na hukipendi, anza kubadilika ndani yako. Anza kubadili fikra zinazotawala akili yako muda mrefu na utabadili unachotoa.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu siyo bahati mbaya, bali ndivyo ulivyo, fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/15/2207

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma