Jambo lolote unalokuwa umejipangia kufanya halafu ukaliahirisha, maana yake ni kwamba umejiambia una jambo jingine muhimu zaidi la kufanya.

Sasa hebu angalia mwenyewe, pale unapoahirisha jambo, ni nini unaenda kufanya?

Mara nyingi unajikuta ukifanya mambo ya hovyo na yasiyo na tija kabisa. Badala ya kukamilisha kazi muhimu, unakimbilia kufuatilia habari au mitandao ya kijamii.

Jambo lolote unaloshawishika kuahirisha huwa ni gumu na mambo magumu ndiyo yenye manufaa zaidi.

Jikamate unapotaka kuahirisha na pima umuhimu wa unachotaka kuahirisha na kile unachokwenda kufanya na ona maamuzi yapi ni sahihi.

Mara zote fanya kilicho sahihi na siyo kilicho rahisi.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu nia njema inapoleta matokeo mabaya, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/21/2213

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma