
Unajifunza mengi unaposhindwa kuliko unaposhinda.
Kushindwa kunakuonesha ni maeneo yapi una udhaifu, wapi bado hujawa vizuri na hivyo kulazimika kujifunza na kukazana uwe bora zaidi.
Kushinda kunakufanya ujione uko vizuri, unajua kila kitu na hilo linapelekea uwe na kiburi kinachokupelekea kuanguka na kushindwa.
Mara kwa mara jiweke kwenye mazingira ya kushindwa, fanya mambo mapya na ambayo hujazoea, fanya makubwa kuliko ulivyozoea kufanya na hayo yote yatakuonesha ni wapi haupo vizuri ili ujiboreshe na kukua zaidi.
Usijisifu kwamba hushindwi, bali jua unafanya mambo madogo na uliyoyazoea na hivyo huwezi kukua zaidi.
Ukuaji upo kwenye kushindwa.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kutowazuia watoto kushindwa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/22/2214
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma