Mtu anayekutana na ukurasa wa leo tu, ambaye hajui kwamba hizi kurasa huwa ni za mfululizo, anaweza kushangaa kwa nini hiyo namba ina mbili nne.
Anaweza kuja na hadithi kuhusu namba hiyo na mengine mengi. Anaweza kuihusisha na imani fulani. Lakini hayo yote ni kwa sababu hajui kilicho nyuma ya namba hiyo.
Hii inaonesha jinsi binadamu tunavyochukulia yale tusiyoyaelewa, kuliko tukae na kitu ambacho hatukielewi, tunajitengenezea hadithi ya kujiridhisha kwenye kile tusichoelewa.
Hivyo ndivyo imani na miiko mbalimbali inavyozaliwa, mwanzo kama hadithi za kujiridhisha ila baadaye inachukuliwa kama ni kweli. Kwa kuwa wote wanaopokea hawahoji kuhusu ukweli au uhalisia wa kitu, wanachukua kama walivyopewa.
Somo kubwa kabisa tunalojifunza hapa ni nguvu yetu katika kutengeneza hadithi za kuturidhisha halafu baadaye tunazisahau ni hadithi na kuanza kuziamini.
Hivyo pia ndivyo miungu mbalimbali imekuwa ikitengenezwa, mwanzo kama hadithi za kujiridhisha na baadaye kama imani ya kusimamia.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,