
Uwezo wetu wanafamu wa kufikiri, ndiyo chanzo cha maendeleo yote duniani. Kila unachokiona kwa macho yako leo, kilianza kama fikra kwenye akili ya mtu.
Na hazikuwa fikra za kawaida, kabla ya vitu hivyo kuwepo, wengi waliamini haviwezekani. Wale waliofikiri vitu hivyo, walionekana kama wamechanganyikiwa au wanaota tu.
Lakini hawakukata tamaa, waliendelea kuamini fikra hizo na leo hii tunayaona matunda yake. Kila maendeleo yaliyopo duniani, yalianzia kwenye fikra.
Je ni fikra gani za tofauti ulizonazo wewe na umekuwa unazificha kwa sababu wengine hawazielewi? Usizipoteze kabisa fikra hizo, badala yake zifanyie kazi ili dunia iweze kunufaika.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kura unazopiga kila siku, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/31/2223
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma