
Inapokuja kwenye matatizo ya wengine, ni rahisi sana kuwashauri, huwa hatukuso chochote cha kuwaambia.
Lakini inapokuja kwenye matatizo yetu wenyewe, tunajikuta tumekwama na hatujui nini cha kufanya.
Hiyo ni kwa sababu tunakuwa tumeweka hisia zaidi kwenye matatizo yetu na hisia zinapokuwa juu, fikra zinakuwa chini.
Unapokuwa kwenye matatizo yoyote yale, kabla hata hujakimbilia kuchukua ushauri wa wengine, anza kujishauri kwanza wewe mwenyewe.
Jione kama ni mtu mwingine ana matatizo hayo na unamshauri. Hili ni zoezi gumu na linalohitaji utulivu mkubwa, lakini ukiweza kulikamilisha, utajipa ushauri bora mno, kwa sababu wewe unajijua kuliko wengine wanavyokujua.
Chukulia kama unamshauri mtu mwingine, jipe utulivu wa kutosha na liangalie tatizo bila ya hisia, majibu mazuri tayari yako ndani yako, ni wewe tu kuyafikia.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kumeza na kufyonza, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/05/2228
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma