Kitu pekee ambaa uhakika nacho kwenye maisha ni kwamba kila mmoja wetu atakufa, itakuwa lini hiyo ndiyo siri ambayo siyo rahisi mtu kung’amua.
Sasa kwa kuwa hatujui hilo litatokea lini, wengi wamekuwa wanaishi kwa hofu kubwa, kitu ambacho kinakuwa ukomo kwao kuyaishi maisha yao kwa ukamilifu wake.
Kwa kuhofia kifo, watu wamejizuia kufanya mambo makubwa na ya tofauti.
Wengine kwa kuona watakufa, wanaona haina haja ya kujisumbua.
Lakini kifo hakipaswi kuwa ukomo, badala yake kinapaswa kuwa uhuru.
Kwa kujua kwamba utakufa, unapaswa kuwa huru kuishi maisha yako, kuiishi kila siku kama ndiyo siku ya mwisho kwako, kutokuahirisha chochote.
Kwa kujua utakufa, unapaswa kufanya kitu kitakachokufanya usisahaulike haraka.
Kwa kujua siku zako zina ukomo, unahakikisha hupotezi muda kwa lolote lisilokuwa muhimu.
Uzuri tuna ushahidi mwingi kwenye hili, kuna watu waliishi maisha yao kwa uzembe, lakini walipoambiwa wamebakiwa na siku chache za maisha, walichagua kuishi tofauti na hatimaye kuacha alama kubwa.
Kila mmoja wetu kuna alama anaweza kuacha hapa duniani, kama atakitumia kifo kama kitu cha kumweka huru badala ya kitu cha kumpa ukomo.
Chagua leo kuwa huru, chagua leo kuiishi kila siku yako kwa ukamilifu, iishi kama siku ya mwisho kwako na ukipata nyingine ni zawadi kwako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ni kweli, hofu ya kifo imewafanya wengi kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu. Sitakubali kifo kinipe ukomo kwenye maisha yangu.
Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Watu wakijua unahofia Sana kifo, watatumia mwanya huo kukutaka ukubaliane na vitu ambacho siyo sahihi kwako kufanya. Sitakuwa na hofu ya kifo kwa sababu ni kitu ambacho Nina uhakika nacho.
LikeLike
Hakika.
LikeLike