
Watu wawili wanapogombana au kutokuelewana, jua kila mmoja amechangia kwa namna fulani pale walipofikia.
Japo ukisikiliza upande mmoja mmoja, utasikia kila upande ukilaumu upande mwingine na upande huo kuonekana ni sahihi.
Lakini utakuwa umefanya makosa makubwa kama utasikiliza upande mmoja pekee, kwa sababu kila jambo huwa lina pande mbili.
Kabla ya kufanya maamuzi, hakikisha umezipata pande mbili za jambo husika.
Hata kama ni biashara unapanga kuanzisha, usifanye maamuzi kwa kuangalia upande wa faida pekee, bali pia angali upande wa hasara na hatari zake, hilo litapelekea maamuzi yako yawe bora zaidi.
Kila jambo lina pande mbili, zijue kabla hujafanya maamuzi.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu watu wa kuwakera, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/12/2235
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma