
Huwa unapanga kufanya kitu, halafu sababu zinaingilia na wewe unaruhusu sababu hizo ziwe kikwazo.
Tatizo kubwa zaidi linakuja pale sababu inapokuwa hiyo hiyo kila siku, miaka nenda miaka rudi, sababu ni ile ile.
Mfano husomi vitabu kwa sababu huna muda, miezi inakwenda, husomi na sababu ni hiyo hiyo kwamba huna muda.
Hivi unadhani kuna siku utaamka na ukute una muda zaidi ya masaa 24 kwa siku?
Tunachoweza kusema hapo ni kwamba kusoma siyo kitu muhimu kwako, ndiyo maana unaruhusu sababu.
Kadhalika kwenye mipango mingine unayojiwekea kama kuanzisha au kukuza biashara, kuboresha mahusiano na afya yako.
Kama kila siku unajipa sababu zile zile, ni vyema tu ukaachana na sababu hizo na kujiambia ukweli kwamba hutaki kufanya kitu hicho ili uache kusingizia sababu hiyo.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu mtu wa kumpa lawama, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/14/2237
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma