Huwa tunashangaza, vitu vya thamani tunavichukulia poa, ila visivyo vya thamani tunahangaika navyo kweli.

Fikiria muda unaotumia kwenye mambo yasiyo na manufaa yoyote kwako, kuanzia kufuatilia habari, maisha ya wengine, mabishano na ushabiki wa kila aina.

Unayapa mambo hayo muda kuliko unavyoweka kwenye vitu vyenye tija kama kujifunza au kufanya kazi yako kwa ubora.

Mstoa Seneca anasema huwa tuna ufujaji wa kitu ambacho tungepaswa kuwa na ubahili mkubwa, ambacho ni muda.

Vitu vingi ulivyonavyo ukivipoteza unaweza kuvipata tena, lakini siyo muda, ukipotea huwezi kuupata tena.

Jali na linda sana muda wako, ni kitu chenye thamani kubwa kwako.

Ukurasa wa kusoma ni mhimili ulioyumbishwa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/23/2246

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma