Unapogundua kwamba upo kwenye hali ya kusukumwa na husia zaidi kuliko fikra, basi jicheleweshe.

Hisia zina tabia ya kukufanya uone unapaswa kuchukua hatua mara moja, ila hatua unazochukua ukiwa kwenye hali hiyo huwa siyo nzuri kwako.

Ukiwa kwenye hasira chelewa sana kuchukua hatua yoyote ile, jipe muda zaidi. Hasira zitakaposhuka utajionea mwenyewe jinsi ulichotaka kufanya hakikuwa sahihi.

Chelewa kujibu pale unapokuwa kwenye majibizano au mabishano na watu wengine, itakuepusha kujibu yasiyo sahihi.

Matatizo mengi kwenye maisha yako yametokana na kufanya au kusema kwa haraka, bila ya kujipa muda wa kutosha kufikiri kwa kina kabla ya kufanya au kusema jambo husika.

Jicheleweshe pale hisia zinapokuwa juu na utaepuka makosa mengi.

Ukurasa wa kusoma ni uchaguzi wa pili muhimu kwenye maisha yako, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/24/2247

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma