
Unapoanguka, hupaswi kubaki pale ulipoangukia, badala yake unapaswa kuinuka na kuendelea na safari yako.
Kila mtu kwenye maisha huwa anaanguka, wanaobaki walipoanguka wanashindwa na wanaoinuka na kuendelea wanafanikiwa.
Na hilo halitatokea mara moja, bali litajitokeza mara nyingi, hata ukianguka mara 10 amka mara ya 11 na uendelee na safari.
Kama bado upo hai, kila dakika unapaswa kupambania kusudi na ndoto zako kubwa, usikubali chochote kiwe kizuizi kwako.
Dunia ina tabia ya kuwapima watu, ili kujua wamejitoa kiasi gani kifanikiwa, inawajaribu kwa namna mbalimbali, hakikisha wewe huangushwi na jaribu lolote.
Kila unapoanguka, inuka, jitathmini na songa mbele.
Ukurasa wa kusoma ni kuongeza ufanisi na uzalishaji wako, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/26/2249
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma