Watu wengi wamekuwa wanapoteza kile wanachokihitaji, ili kupata wasichohitaji na mwisho kujikuta wameanguka vibaya.

Hiyo yote husababishwa na tamaa ya kutaka kupata zaidi au kutokutaka kupitwa na kile ambacho wengine wananufaika nacho.

Warren Buffett anaita huu ni upumbavu wa kiwango cha juu na ndiyo unapelekea wengi kuanguka kwenye biashara na uwekezaji.

Mfano una biashara yako unayoiendesha vizuri, una wateja wanaokuamini na kukutegemea na unaingiza faida kiasi cha kutosha kuendesha maisha yako.

Unasikia kuna fursa mpya imejitokeza, ambapo ukiweka fedha zako unapata faida mara mbili ndani ya miezi mitatu. Unaondoa kiasi kikubwa cha mtaji kwenye biashara na kuwekeza kwenye hiyo fursa mpya.

Kumbe ni utapeli, hakuna faida unapata na umepoteza uwekezaji uliofanya. Huku biashara yako iliwa imeathirika sana na hata kufikia kufa kwa sababu haina mtaji wa kutosha.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu yasiyoonekana unayoyapuuza, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/27/2250

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma