Wachezaji wa mpira wa miguu, huwa wanaelekeza mpira kwenye goli la timu pinzani.

Siyo mipira yote inaingia na kufunga goli, lakini mara chache mpira utaingia golini na kuwa wamefunga goli, kitu kinachowaweka kwenye nafasi ya kupata ushindi.

Kama wataelekeza mipira sehemu nyingine ambayo siyo goli la timu pinzani, hawawezi kushinda kabisa.

Hakikisha unalenga kilicho sahihi kama kweli unataka kukipata. Kabla hujaweka juhudi kubwa, hakikisha kwanza uelekeo ni sahihi.

Na ukishakuwa kwenye uelekeo sahihi, wewe kazana na mchakato, matokeo yatakuja kwa wakati wake.

Ukurasa wa kusoma ni yanayoonekana kwa urahisi kwa waliofanikiwa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/28/2251

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma