
Hofu ya kushindwa ni moja ya vikwazo vinavyowazuia wengi kuchukua hatua na hata kuwakatisha tamaa wanapokutana na magumu.
Wewe usijiulize unawezaje kuvuka magumu unayokutana nayo, bali jiulize magumu yanawezaje kukushinda.
Kwa kubadili mtazamo wako kwa namna hiyo, unabadili kabisa mwelekeo wa maisha yako.
Kushinda kunakuwa hakuna nafasi kwako, haijalishi unakabiliana na nini, utaendelea kupambana mpaka upate unachotaka.
Kuamini kwamba utaweza kupata unachotaka bila kujali unapitia nini, ni hitaji muhimu kwa mafanikio yako.
Ukurasa wa kusoma ni kukosa msimako kunavyokuchelewesha kufanya maamuzi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/01/2252
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma