Mwili wako huwa haupendi kuchoka wala kuumia, hivyo hutafuta kila mbinu kukwepa kufanya mambo magumu.

Hufanya hivyo kwa kuishawishi akili kwamba mambo ni magumu na hayawezekani.

Iwapo akili itautii mwili wako, hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Badala yake akili inapaswa kuusukuma mwili uende zaidi, akili inapaswa kuupa mwili nguvu zaidi.

Hilo linawezekana pale unapokuwa na kwa nini na shauku kubwa kwenye kile unachokifanya.

Lazima uusikilize mwili, kwa sababu kuna vitu muhimu unakuambia, lakini hupaswi kufuata kila ambacho mwili unataka, maana vingine ni uvivu na uzembe tu.

Hakuna aliyefanikiwa kwa kuusikiliza na kuutii mwili kwenye kila kitu. Mwili lazima usukumwe zaidi ya unavyotaka wenyewe.

Ukurasa wa kusoma ni wakati sahihi wa kuvuka daraja, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/03/2254

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma