Yale unayoona yakitokea kwenye maisha ya wengine, jua na kwako pia yanaweza kutokea. Iwe ni mazuri au mabaya, yana nafasi ya kuja kwako pia.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi sahihi ya kukabiliana na lolote linalokuja kwako, ili lisikujie kwa mshangazo.

Mstoa Seneca alishauri mtu uishi kwenye ile hali unayoihofia kutokea na utajionea mwenyewe kwamba hakuna cha kuhofia sana.

Kama unahofia kazi au biashara yako ikifa hutakuwa na fedha ya kuendesha maisha yako, mara moja moja ishi maisha yako kama vile huna kazi au biashara yako.

Ishi kwa hadhi ya chini kabisa katika siku unazochagua na jiulize kipi cha kuhofia sana katika maisha hayo.

Hupaswi kuhofia yajayo, unapaswa kuwa na maandalizi ya kukabiliana na chochote.

Ukurasa wa kusoma ni hatujui dunia ina nini kwa ajili yetu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/06/2257

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma