
Matatizo, vikwazo na changamoto mbalimbali unazopitia kwenye maisha yako, ni asili inakuadhibu.
Asili huwa ina sheria zake ambazo huwa haiziweki wazi, lakini unapozivunja, inakupa adhabu kali.
Kwa kila gumu unalopitia kwenye maisha, jiulize ni sheria ipi ya asili unaivunja, ijue, ifuate sheria hiyo na utaondokana ba magumu hayo.
Asili haina huruma, inafuata sheria zake bila kujali nani anazikubali au hazikubali, usishindane nayo, zijue sheria za asili, zifuate na uwe na maisha bora.
Ukurasa wa kusoma ni kutokujua sheria siyo kinga ya kutokuadhibiwa na sheria hiyo, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/12/2264
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma