
Bondia akiwa ulingoni, anaweza kutumia mbinu ya kumkimbia adui ili kujipa muda wa kumsoma adui na kuweka mkakati wake.
Lakini lazima amkabili na kumshambulia kama anataka ushindi.
Hawezi kushinda kwa kukimbia pekee na akikimbia sana ataishia kuchoka na kushindwa kirahisi.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa matatizo na changamoto mbalimbali za maisha, unaweza kuzikimbia kwa muda kama unatumia muda huo kuzisoma na kujipanga zaidi.
Lakini kama unazikimbia kwa kuamini zitaondoka, unajidanganya, kwani hapo unazipa nafasi ya kukua zaidi.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu unaposimama wewe, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/15/2266
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma