
Mambo ya kufanya ni mengi ma mengi mno yanawinda umakini wako. Lakini huna muda wala nguvu za kuweza kufanya yote yanayokutaka uyafanye.
Kama unataka matokeo mazuri, lazima uweke vipaumbele vyako vizuri, uhangaike na yale ambayo ni muhimu zaidi, ambayo wewe tu ndiye unaweza kuyafanya kwa namna bora unayotaka.
Mengine ambayo yanaweza kufanywa na wengine, tafuta wanaoweza kuyafanya vizuri na kisha walipe vizuri wayafanye.
Malipo unayowapa wengine wakusaidia ya kufanya ni malipo unayotumia kununua muda na nguvu zaidi kwa ajili yako.
Usihangaike na kila kitu, maana itakuchosha na kupoteza muda wako mwingi.
Ukurasa wa kusoma leo ni kazi yako ni pesa na madili, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/20/2271
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma