Uadilifu ni moja ya misingi muhimu sana kwenye mafanikio yako.

Ili ufanikiwe, lazima watu wakuamini na watu watakuamini kupitia uadilifu wako.

Huwezi kuaminika kama unayosema na unayofanya yanatofautiana.

Huwezi kuaminika kama unaahidi vitu na hutekelezi.

Huwezi kuaminika kama ukiwa faragha unafanya mambo mengine na ukiwa kwenye hadhara unafanya mambo mengine.

Uadilifu ni kuwa na maisha ya aina moja na kuyaishi wazi, kutokuwa na chochote unachoficha kwenye maisha yako.

Safari ya mafanikio tayari ni ngumu, kuwa na maisha ya aina zaidi ya moja kwa sababu huna uadilifu itazidisha ugumu wa safari yako na kuwa kikwazo kwa mafanikio yako.

Simamia msingi huu wa uadilifu, upunguze ugumu wa safari, uaminike na wengine na uweze kufanya makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni kushindwa kwa kujitakia, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/23/2274

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma