Safari ya mafanikio siyo rahisi, inahitaji mapambano makubwa.

Hivyo hitaji la kwanza muhimu kwenye safari hii ni mtu kuwa na afya imara.

Afya hiyo inahusisha mwili, akili na roho. Akili inafanya maamuzi, roho inakupa msukumo na mwili unayekeleza.

Kwenye afya ya akili unapaswa kuilisha maarifa sahihi, roho inahitaji utulivu mkubwa na mwili unahitaji kula vizuri, mazoezi na kupumzika.

Unapaswa kuweka kipaumbele cha kwanza kwenye afya yako maana bila hiyo hakuna kingine kitakachowezekana.

Kila maamuzi unayofanya, angalia yanaathirije afya yako.

Ukurasa wa kusoma ni kushika tamaa za watu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/25/2276

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma