
Kuna watu wakisikia neno utajiri wanajisikia vibaya, kama vile ni neno baya ambalo ni mwiko kulisema hadharani.
Hivyo ndivyo jamii ilivyowatengeneza watu, kuhakikisha hawafikii utajiri ili waendelee kuwa watumwa wa jamii husika.
Utajiri ni kitu cha asili, asili huwa haipendi utupu, hivyo hujaza kila aina ya utupu.
Fikiria madini ambayo yamekuwa yanachimbwa miaka na miaka lakini hayaishi.
Fikiria samaki ambao watu wamekuwa wanakula lakini bahari na maziwa hayaishiwi.
Hapo unajionea mwenyewe jinsi asili inavyojenga utajiri.
Na wewe pia unaweza kujenga utajiri ukizifuata kanuni za asili, kama kutoa thamani zaidi, kuweka akiba na kuwekeza, kujipa muda na kuwa na uvumilivu.
Utajiri ni moja ya miongozo unayopaswa kutumia katika kuweka vipaumbele vyako.
Utajiri ni mzuri, utajiri ni haki yako, upende utajiri na fanyia kazi kufikia utajiri.
Ukurasa wa kusoma ni kuchaji betri, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/26/2277
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma