Kujua pekee haitoshi, bali kufanyia kazi kile unachojua ndiko kunakoweza kukufikisha kwenye mafanikio.

Hekima ni kujua na kufanyia kazi kile unachojua. Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna uhaba wa maarifa, lakini kuna uhaba mkubwa wa hekima.

Watu wamekuwa wanapata maarifa mengi, lakini hawawezi kuyachambua na kujua yaliyo muhimu na kisha kuyatumia kuyaboresha maisha yako.

Wewe jijengee hekima, kwa kujua yale muhimu kwa unachotaka na kisha kuchukua hatua kwa yale unayojua.

Usifurahie tu kujifunza na kujua, bali jiulize unayatumiaje yale uliyojifunza na kuyajua?

Hata ukifanyia kazi machache tu kati ya yale unayojua sasa, inatosha kukuwezesha kupiga hatua kubwa.

Anza sasa kufanyia kazi yale unayojua na utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Ukurasa wa kusoma ni kutokuwa mtu wa kawaida, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/27/2278

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma