Kama kuna rafiki mmoja unayemhitaji sana kwenye maisha yako basi ni kazi. Kazi haijawahi kumtupa yeyote anayeipenda na kuiheshimu.

Kazi imekuwa inalipa sawasawa na mtu anavyoweka juhudi. Chochote unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kupitia kuweka kazi kwa juhudi kubwa. Kuanzia fedha, mafanikio, heshima, afya na hata mahusiano bora.

Kila chenye thamani kwenye maisha ni matokeo ya kazi. Kuwa tayari kuweka kazi, ipende na kuiheshimu kazi na itakuwa tayari kukupa chochote unachotaka.

Kumbuka asili huwa haipendi madeni, hivyo inahakikisha inakulipa sawasawa na kazi unayoweka.

Ukurasa wa kusoma ni maswali matano ya kukupa mwanga; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/28/2279

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma