
Wengi hufikiri uhuru ni kutokuwa na ukomo wowote, lakini hiyo siyo sahihi.
Kila kitu kwenye asili kina ukomo wake. Chukua mfano wa muda, kila mtu ana masaa 24 tu kwenye siku yake, hakuna anayeweza kuongeza hata sekunde moja ya ziada.
Lakini kuna watu wana uhuru mkubwa wa muda, kwa kuwa wanajua jinsi ya kupangilia vizuri muda wao wenye ukomo.
Uhuru ni pale unapoweza kuchagua jinsi utakavyotumia ukomo ulionao.
Kwa kutambua ukomo unaokukabili na kuupangilia vizuri, utaweza kuwa huru na kufanya makubwa.
Utawasikia wengi wakilalamikia ukomo unaowakabili, usijiunge nao, wewe angalia kipi unaweza kumiliki kwenye ukomo huo na kifanyie kazi.
Uhuru siyo kitu unachoweza kupewa na yeyote, bali kitu unachochagua wewe mwenyewe.
Chagua kutumia ukomo ulionao vizuri ili kuwa huru.
Ukurasa wa kusoma ni hataki au hawezi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/01/2283
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma