
Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, tumejengewa mazoea ya kutaka kuwaridhisha wengine ili watukubali.
Hili lilikuwa muhimu kipindi cha kale ambapo watu walikuwa kwenye makundi madogo na hali ilikuwa hatari.
Lakini sasa mambo yamenadilika, hatupo tena kwenye makundi madogo na hatari siyo kubwa.
Hivyo unapokazana kuwaridhisha wengine, haina msaada wowote kwako, kwa sababu hautaweza kumridhisha kila mtu na utashindwa kuyaishi maisha yako.
Mtu wa kwanza unayepaswa kumridhisha kwenye maisha ni wewe, kisha wengine wachague kama wataweza kwenda na wewe au la.
Ukurasa wa kusoma ni hatari za kipumbavu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/02/2284
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma