
Kuna wakati utaweka juhudi na muda kwenye kile unachofanyia kazi, lakini matokeo unayopata yasiwe sahihi.
Ni rahisi kuona juhudi na muda ulioweka vimepotea. Kama upo kwenye mchakato sahihi, basi jua hakuna kinachopotea, hata kama matokeo unayopata siyo uliyotaka, jua juhudi na muda ulioweka havijapotea, badala yake ni uwekezaji ambao baadaye utakupa matokeo mazuri.
Muhimu ni kuhakikisha uko kwenye mchakato sahihi, kisha usikate tamaa mpaka umepata kile unachotaka.
Ukurasa wa kusoma ni vipengele vitano vya mchakato wa mafanikio; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/09/2291
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma