Mambo mengi, muda mchache ni kauli maarufu sana enzi hizi.

 Mambo yakufanya yanaongezeka kila siku, lakini muda wa kufanya mambo hayo ni ule ule.

Na hapa ndipo wengi wanapopata msongo.

Ili tuweze kuondokana na usumbufu kwenye maisha yetu, tunapaswa kutenga muda wa kufanya yale ya muhimu kwetu na kuuheshimu muda huo.

Watu wengi wamekuwa hawatengi muda wa kufanya vitu , huwa wanaona muda upo tu, wanakuja kushtuka siku imeisha na hakuna kikubwa ambacho wamekifanya.

Kama unataka kuondoa usumbufu kwenye maisha yako , unapaswa kutenga muda wa yale muhimu kwenye maisha yako, na kisha kutumia muda huo kwa yale uliyopanga tu, na siyo kwa jambo jingine lolote.

Lakini pia unapaswa kutenga muda kwa ajili ya usumbufu, na kila aina ya usumbufu unauruhusu kwenye muda huo.

 Unapotenga muda kwa ajili ya vitu na kuuheshimu, utaweza kukabiliana na usumbufu na kufanya makubwa.

Swali ni je unapangaje muda na tunawekaje vipaumbele vyetu?

Kuna maeneo matatu(3) muhimu kwenye maisha yetu, maeneo ambayo ndiyo tunapaswa kuyapa kipaumbele kwenye muda wetu.

Maeneo hayo ni wewe binafsi, mahusiano na kazi.

Ndani ya kitabu kipya kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utakwenda kujifunza jinsi ya kuweka vipaumbele kwenye maeneo hayo matatu na kuondoka na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na  kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

 Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

 Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

 Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

OFA: Ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi unaosomeka “NIUNGE” kwenda namba 0752977170, baada ya kununua kitabu chako.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.