
Huwa tunapenda kupima usahihi wa kitu kwa kuangalia wingi wa wanaokifanya.
Kama wengi wanafanya au kukubaliana na kitu, tunaamini kitu hicho ni sahihi na hata kama siyo sahihi basi tunaamini kifo cha wengi ni harusi.
Tatizo ni huwezi kufanikiwa kwa kuhangaika na yasiyo sahihi na kama unapima usahihi wa kitu kwa wingi wa wanaokifanya, hutafika kwenye kufanya kitu sahihi kwa sababu vilivyo sahihi siyo rahisi na wengi hawapendi visivyo sahihi.
Pambana kutambua usahihi wa kitu kwa misingi yake na siyo kwa kuangalia wanaokifanya.
Ukurasa wa kusoma ni tatizo la wataalamu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/12/2294
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma