
Watu watajitolea kukupa ushauri mbalimbali ambao hata hujawaomba.
Wataona wanajua jinsi unavyopaswa kuyaishi maisha yako kuliko wewe unavyojua. Chunga sana usishawishiwe na kila ushauri watu wanakupa.
Kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako ni kupata kile unachotaka na hivyo ushauri unaohitaji ni wa kukusaidia kufika huko.
Kama bado hujapata unachotaka, ushauri usiolenga kukufikisha huko ni kelele tu kwako.
Ukurasa wa kusoma leo ni kama bado hujapata unachotaka; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/18/2300
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma