
“A man with outward courage dares to die; a man with inner courage dares to live.” – Lao Tzu.
Kuishi kunahitaji ujasiri wa ndani, kufa kunahitaji ujasiri wa nje. Wengi wanauweza ujasiri wa nje, lakini wachache mno ndiyo wanauweza ujasiri wa ndani, kuweza kuyaishi maisha yao.
Utasikia mtu anasema niko tayari kufa kwa ajili ya kitu fulani, wakati mtu huyo hajawahi kuwa na ujasiri wa kuyaishi maisha yake.
Kila mtu atakufa, huna haja ya kujivunia hilo.
Wachache sana ndiyo wanayaishi maisha yao, kuwa mmoja wao.
#MementoMori #ThubutuKuishi #KochaMakirita