Chochote unachorudia kufanya kwa muda mrefu, huwa unakijengea tabia na kuanza kukifanya kwa mazoea. Inafika wakati unakifanya bila hata ya kufikiria kabisa.

Ni vizuri kwa akili yako maana inapunguza mengi ya kufanya, lakini ni mbaya kwa ubunifu na ufanisi.

Ukishafanya kwa mazoea huwezi kuja na ubunifu mpya. Kwa kuwa mazoea lazima yajengeke, ni wajibu wako kuhakikisha unayavunja ili ifanye kwa usahihi.

Mara kwa mara jifanyie tathmini na kuona wapi unafanya kwa mazoea kisha yavunje. Usipofanya hivi, utajikuta unapambana sana, lakini hupigi hatua kubwa.

Ukurasa wa kusoma ni alama tatu za umasikini; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/22/2304

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma