2306; Hadhi inaanzia mfukoni…
Kuna watu hawana fedha, lakini wakishauriwa hatua za kuchukua ili watoke kwenye hali hiyo ya kutokuwa na fedha huwa wanaleta ubishi.
Wanasema hawawezi kuchukua hatua hizo kwa sababu zitashusha hadhi yao.
Iko hivi rafiki, kama huna fedha, hakuna njia halali ya kuingiza fedha ambayo siyo ya hadhi yako.
Ungekuwa kweli na hiyo hadhi unayosema, tayari ungekuwa na hizo fedha unazotaka.
Ila huna fedha hizo, ilimaanisha huna hadhi unayojipa.
Linapokuja swala la fedha, weka juhudi kupata fedha na weka hadhi pembeni.
Uzuri ni ukishakuwa na fedha, hakuna anayejali umeipata kwa kazi yenye hadhi gani.
Ukienda kununua kitu, huulizwi ulifanya kazi ya hadhi gani ukapata fedha hiyo.
Kadhalika unapowasaidia wengine au kutoa sadaka.
Watu wanachotaka ni fedha yako, hawataki kujua hadhi ya ulichofanga kuipata.
Hivyo weka hadhi pembeni na pata fedha. Chochote kilicho haki kufanya, kilicho ndani ya sheria na hakivunji maadili, kifanye.
Ukishaipata fedha, itakuza zaidi hadhi yako.
Kocha.