Utakapochagua kuishi maisha ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa, watu wanaokuzunguka hawatapendezwa na hilo.

Watakupinga, kukukatisha tamaa na hata kukushauri namna unavyopaswa kuyaishi maisha yako.

Cha kushangaza sasa, watu hao hawajui hata wanavyopaswa kuyaishi maisha yao, lakini wanaona ni wajibu wao kukupangia wewe jinsi ya kuishi.

Kama utawasikiliza watu hao, utakuwa umekwenda na maji, hutaweza kufanikiwa, utaishia kama wao.

Ukisikiliza ushauri wa mtu ambaye hajafanikiwa au hayupo kwenye njia ya kuelekea kwenye mafanikio, utaishia kuwa kama yeye.

Hivyo kuwa makini na ushauri ambao wengi wapo tayari kukupa kabla hata hujawaomba, ni wa kukupoteza.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu vitu vinne vinavyoathiri kipato chako; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/23/2305

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma