
Ni kufanya mambo rahisi, kuishi kwa mazoea na kuigiza maisha.
Unafanya mambo rahisi kwa sababu hutaki kuchoka, kusumbuka wala kuumia, hutaki pia kushindwa.
Unafanya kwa mazoea kwa sababu hutaki kufikiri tofauti na unahofia kujaribu vitu vipya kwa kuwa huna uhakika navyo.
Unaigiza maisha kwa kutaka uonekane tofauti na uhalisia wako ulivyo, huna fedha lakini unataka wengine waone una fedha na hapo unaishia kuwa na madeni makubwa.
Hatua ya kwanza na muhimu kuondokana na ugumu wa maisha ni kuishi maisha ya uhalisia kwako mwenyewe, halafu kufanya mambo magumu na kuachana na mazoea.
Ukurasa wa kusoma ni hadhi inaanzia mfukoni; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/24/2306
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma