2313; Maamuzi Ya Kamati…

Huwa kipo kichekesho kwamba kamati ni kikundi cha watu wasio na uwezo na ambao hawapo tayari waliopewa jukumu lisilokuwa muhimu.

Maamuzi yanayofanywa na kamati ni yale ambayo mtu mmoja hataki kulaumiwa kwa maamuzi anayofanya.
Hilo hupelekea maamuzi yanayofikiwa na kamati kuwa ya kubembelezana na siyo yanayosimamia ukweli.

Hakuna mmoja aliye tayari kuwajibika kwa matokeo na hivyo kukubaliana na wengine hata kama kitu siyo sahihi.
Kipaumbele kinakuwa siyo kusimamia ukweli, bali kuwaridhisha wengine.

Hakuna maamuzi bora na muhimu yanayofanywa na kamati. Hata pale kamati zinapokuwepo, huwa zinatumika tukupitisha maamuzi yaliyofanywa na wachache.

Hivyo kwa mambo yako binafsi, iwe ni biashara yako au mengine yaliyo chini yako, epuka sana kutumia kamati.

Wanasema hakuna kibaya kisichokuwa na uzuri wake, uzuri wa kamati ni kurefusha mambo na kutumi fedha.

Unaona hapo wazi kwa nini unapaswa kuepuka sana kamati, kwa sababu zinakupotezea muda na fedha pia.

Maamuzi makubwa na muhimu yanapaswa kufanywa na mtu mmoja au watu wachache wanaojua kile hasa wanachofanya na kujua wapi wanataka kufika.

Kamati ni nji ya kujificha pale ambapo mtu hawezi au hathuhutu kuchukua hatua fulani.

Kuwa sana na hili.

Kocha.