
Maamuzi ya kufanya kwa makubaliano ili kumridhisha kila mtu huwa maamuzi mabovu sana kwako.
Maamuzi yoyote yanayofikiwa na kundi kubwa la watu huwa ni maamuzi ya kawaida na hata utekelezaji wake huwa siyo mzuri.
Maamuzi yanapaswa kusimama kwenye ukweli na siyo kumridhisha kila mtu.
Ili ufanikiwe, lazima uwe tayari kufanya maamuzi hata pale ambapo wengine hawayaelewi.
Kwa kuwa hawaoni unachoona mbele na pia hawana uthubutu wa kukabili hofu kama ulionao wewe.
Wanaofanikiwa sana ni wachache kwa kuwa ndiyo wanaoweza kufanya maamuzi yao wenyewe na siyo kutegemea au kutaka kuridhisha kundi.
Ukurasa wa kusoma ni maamuzi ya kamati; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/01/2313
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma