Kazi ndiye rafiki wa kweli, rafiki atakayekufikisha kwenye mafanikio makubwa lakini pia asiyekuwa na wivu wala kukatisha tamaa.

Lakini kazi zote hazifanani, kuna kuifanya kazi husika, kuyasimamia wanaofanya kazi na kumiliki kazi inayofanyika.

Japo zote ni kazi, ila kiwango cha malipo kinatofautiana sana. Wewe kazana uwe mmiliki wa kazi inayofanyika na siyo tu kuwa mfanyakazi, mafanikio na utajiri mkubwa unatokana na umiliki wa kazi.

Na kwa kuwa muda una ukomo, kumiliki kazi kunakuwezesha kununua muda wa wengi kuliko kuwa tu mfanyakazi. Miliki kazi inayofanyika ili ulipwe zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni tofauti za kazi kwenye malipo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/02/2314

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma