
Kutokufanikiwa kwako hakutokani na kukosa rasilimali, bali kunatokana na matumizi mabaya ya rasilimali ambazo tayari unazo.
Mfano rasilimali kubwa kabisa ni muda na nguvu zako. Kila siku una masaa yale yale 24, kama hufanikiwi siyo kwa sababu umepunjwa muda, ila kwa sababu unautumia vibaya, kwa mambo yasiyo na tija.
Kadhalika kwenye nguvu zako, unazitawanya hovyo kwa mambo yasiyo muhimu, mwishowe unachoka na kushindwa kufanya yaliyo muhimu.
Hatua muhimu kuchukua ili kufanikiwa ni kutunza sana rasilimali muhimu ulizonazo, kuhakikisha zinatumika kwa yale muhimu tu na yanayokufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Ukurasa wa kusoma ni uchoshi ndiyo mafanikio; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/03/2315
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma