
Maisha ndiyo haya haya, usiyapoteze kwa kusubiri mpaka kila kitu kiwe tayari ndiyo uanze kuyaishi. Kufanya hivyo ni kuchagua kuyapoteza maisha yako.
Maisha yako tayari yamekamilika kwa ndani, hupaswi kusubiri chochote cha nje ili kuanza kuyaishi. Ishi sasa vile unavyotaka, kwa maisha halisi kwako na chochote unachoona bado hujawa nacho kitakuja kwa wakati sahihi.
Kusubiri mpaka uwe na kila unachotaka ni kuchagua kuyapoteza maisha yako.
Ukurasa wa kusoma ni kitu rahisi kuahirisha; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/06/2318
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma